Saturday, 8 February 2014

MUHADHARA WA TATU: VIPINDI VYA USHIRI WA KISWAHILI
MUDA SAA:
MHADHIRI; KADAWI

VIPINDI VYA USHAIRI.

Chimbuko la ushairi.
Ushairi kama utanzu wa fasihi, chimbuko lake linahusishwa na chimbuko la fasihi na sanaa kwa ujumla, chimbuko la fasihi ukiwemo ushairi ni kazi, na fasihi ya kwanza katika historia ya fasihi ni wimbo wa kazi. Wimbo ni utanzu wa ushairi hivyo tunashawishika kusema kuwa fasihi ya kwanza ni ushairi simulizi.

Ushairi unahusishwa na kazi kwa sababu chimbuko la kazi, hivyo basi kazi ina dhima kubwa katika asili na chimbuko la fasihi ukiwemo ushairi kama utanzu mkongwe kuliko mwingine. Kwa vile fasihi ni sanaa inayotumia lugha, basi lugha ndiyo nyenzo ya sanaa ya fasihi, hivyo basi lugha ina dhima muhimu katika ushairi.

USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA VIPINDI MBALIMBALI
Katika mjadala huu tutatumia mkabala wa kimapokeo kama alivyojadili N.O.MMBAGA, makabala huu si mgeni katika kuchambua historia ya ushairi wa Kiswahili.
Ni muhimu kujua kwamba bara la Afrika si bara la giza bali watu wakeasilimia kubwa ni weusi. Vifuatavyo ni vipindi muhimu sana katika kusoma historia ya ushairi wa Kiswahili;

  1. KIPINDI CHA 1884-1913
Katika kipindi hiki mashairi mengi yaliibuka, wakati huu mashairi yalikuwa ya kiitikadi, itikadi hiyo tunaweza kugawanya katika mafungu yafuatayo:
a.   ya kati na kisimulizi.mfn, Elmandjebu.
      Ya hakiko au ya kishambulizi haya yilipinga ukoloni, mfn, Buhry.
b. mashairi ya kupinga ukoloni  mfano, elkadri
   
c. mashairi ya vibaraka au walamba viatu. Mfn sifa za wazungu.
    
  1. KIPINDI CHA 1918- 1949
Fasihi ya Kiswahili katika kipindi hiki  cha ukoloni wa kiingereza tunaweza kuihakiki chini ya fasihi ya kikoloni, ambayo ilijaa vionjo vya kidini, hii tunaweza kuigawa katika mafungu yafuatayo:
    1. maadili
    2. malimwengu
    3. ya kidini
    4. tafsiri,
            mashairi mengi ya kipindi hiki yalijitokeza katika gazeti la kikoloni lijulikanalo
            kama mambo- leo.
            
Mpangilio huu unafanana kidogo na mpangilio wa Kezilahabi E. katika makala yake ya Uchunguzi katika Ushairi wa Kiswahili FASIHI, TUKI (1983).

Kezilahabi E. anagawanya historia ya ushairi wa Kiswahili katika mihula kama ifuatavyo:

  1. muhula wa urasimu 1128-1885,
katika muhula huu kezilahabi anataja tenzi kama vile
ü      utenzi wa Tambuka (1149) (1690)
ü      utenzi wa Al-inkshafi (1810-1820)
ü      utenzi wa Mwana kupona
ü      utenzi wa Ayubu
ü      utenzi wa Ngamia na paa
ü      utenzi wa Masahibu
ü      utenzi wa Kiyama
ü      utenzi wa mikidadi Mayasa
ü      utenzi wa RasL’ Ghuli
ü      utenzi wa Shufaka
ü      mashiri ya Muyaka bin Haji
ü      mashairi ya Bwana Mutaka na Ali Koti
   
  1. Muhula wa utasa 1885- 1945
Katika muhula huu zipo pia tenzi kama vile:
ü      Utenzi wa vita vya majimaji
ü      Utenzi wa vita vya uhuru
ü       
  1. Muhula wa urasimi Mpya 1945- 1960
Hapa anawataja washairi kama akina Shaaban Robert, Amri Abed, Khamis Amani(Nyamaume), Mathias Mnyampala, Ahmed Nassir, Mdanzi Hanass, Kibwana, Abdi Matunga, M.M Kihere n.k

  1. muhula wa sasa 1967 hadi leo
hapa ingawa hawataji washairi mashuhuri wa kipindi hiki nitawataja wachache miongoni mwao akiwemo Kezilahabi E, M.M. Mulokozi na Kahigi, A. Abdalla n.k

historia ya ushairi wa Kiswahili ina mikabala mingi basi kama ni hivyo endelea kufuatilia muhadhara ujao. Nakutakia kazi njema asante kwa kunisikiliza.
Kwa chanzo muhimu cha habari hii soma – makala za semina ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili III, FASIHI (2003:148-150)


 Tutaendelea.....................

No comments:

Post a Comment