ISTILAHI ZA USHAIRI -
tarehe 8/02/2014
MAANA YA ISTILAHI
Ni
maneno yanayotumiwa katika tathinia fulani, hivyo katika taaluma ya ushairi
kuna istilahi muhimu zitumikazo katika kuunda na kujenga ushairi wa Kiswahili.
Istilahi hizo ni:
- Arudhi
Ni
sheria na kanuni za kimapokeo, jadi au kitamaduni zinazoongoza utunzi
wa mashairi, tenzi, na ngonjera. Kanuni
hizo zaweza kuwa ni vina, mizani,
beti, mishororoau mistari, kituo, kibwagizo,
mikarara, utoshelevu, muwala
na lugha safi .
- Bahari
Ni kina kinachotokeza mwishoni mwa
mshororo wa beti.
- Ubeti
Ni mgawo wa vifungu katika shairi,
utenzi, au ngonjera unaojitosheleza
kimaana.
TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa: ubeti ni kifungu chenye kuleta maana kamili katika jumla ya vifungu
vilivyomo katika utungo.
Mfano:
Kaa kaa kwenye kiti, kaa na kaa wa
pwani,
Kaa ni la moto binti, nisikiza kwa
makini,
Kaa waambiwa keti, ewe bwana una
nini?
Huu ni ubeti mmoja katika utungo wa shairi
letu kutoka katika Mzenga, (2010:4)
- mshororo
ni mstari katika ubeti wa shairi ambao
una maana kamili. Katika mashairi
ya arudhi inatakiwa mistari iwe sawa
kimizani ingawa baadhi ya mashairi
huwa yanakuwa na mizani tofauti.
Mfano:
Paa ni la kuezeka, kwenye nyumba pulikani.
Huu
ni mshororo mmoja wenye mizani kumi na sita.
- mwanzo
ni mshororo wa kwanza katika ubeti wa
shairi. Katika tarbia mshororo wa
kwanza
huitwa ufunguo au fatahi au kifunguo.
Buibui
ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
Kwani naona uchungu, kwa maisha
uishivyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina
stara.
Nyumba iso mlingoti, na wala
vipachikiyo,
Toka pembe hadi kati, yote ya
mning’iniyo,
Haiezekwi makuti, na wala
kifunikiyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina
stara.
Ubeti
wenye wino mzito ni mfano wa mwanzo wetu katika utungo wetu.
- mroto
ni mshororo wa pili katika ubeti wa
ushairi.
Mfano:
Buibui ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
Kwani naona uchungu, kwa maisha
uishivyo,
Mstari
wenye wino mzito kishairi huo ni mroto.
- mleo
ni mshororo wa tatu katika ubeti wa
shairi.
Mfano:
mja deni utalipa, hata likiwa ni mia,
dawa ya deni kulipa, wala siko
kukimbia,
deni harusi kukopa, kulipa wafikiria,
ili moyo uwe shwari, mja kamilisha
deni.
Mleo umekolezwa zaidi ya mishororo mingine
katika ubeti.
- kituo
ni mshororo wa mwisho katika ubeti wa utungo
wa ushairi. Maneno ya kituo
yanaweza yakawa yale yanayokaririwa katoka
ubeti hadi ubeti yaani kibwagizo.
Pia yanaweza kubadilika toka ubeti
wa kwanza hadi ubeti wa pili wa shairi na
kubadilika
huku kunaitwa kimalizio. TUKI (2003:94), wameandika kuwa: kituo ni mstari wa
mwisho katika kila ubeti wa ushairi. Kituo huweza kuwa kimalizio au kiini. Kina
kuwa kimalizio kinapokuwa kuwa kinatumiwa kama
kitu cha kulifunga na kulikamilisha wazo moja katika kila ubeti. Kina kuwa
kiini inapokuwa kikitumiwa na
kikijitokeza katika kila mwisho wa ubeti na kinataja kwa muhtasari jambo muhimu
linalozungumziwa.
Mfano:
(Kapele H. 2013),
Mke bwana mtafute, popote upajuapo,
Tia nia umpate, usikwepe ya malipo,
Raha ya ndoa fungate, fungate pasi
mkopo,
Mke
usije kupewa, matusi atakutia.
Mke ni yako zawadi, zawadi ya
boksini,
Hata kiwa mkaidi, ya ndoa yote
sirini,
Hata akiwa ni udi, usitangaze
mbaoni,
Mke
usije kupewa, matusi atakutia.
Kituo
kimetiwa wino mzito.
- kibwagizo
ni mstari wa mwisho wa ubeti unaorudiwa
katika kila ubeti wa shairi lote, pia
kwa lugha nyingine waweza kuitwa mkarara,
kipokeo au kiitikio. Huweza kuwa
kipande kinachorudiwa katika mshororo wa
mwisho wa ubeti. Kazi ya
kibwagizo katika ushairi yaweza kuwa ni
kusisitiza jambo ambalo msanii na
mtunzi wa shairi amelenga jamii iweze
kulisoma, kulisikia, kulifanya na kuamua pia
kibwagizo
hueleza dhamira muhimu ya shairi katika mengi ndicho huwa kiini na kichwa cha shairi.
Mfano:
TUKI (2003:103)
Buibui ndugu yangu, si numba
uliyo nayo,
Kwani naona uchungu, kwa maisha
uishivyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina stara.
Nyumba iso mlingoti, na wala
vipachikiyo,
Toka pembe hadi kati, yote ya
mning’iniyo,
Haiezekwi makuti, na wala
kifunikiyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina
stara.
Katika
beti hizi kibwagizo kimekolezwa kwa wino zaidi.
- kimalizio
ni
mstari wa mwisho katika ubeti ambao haurudiwi katika kila ubeti, mstari huu
hufanya kazi ya kukuamilisha wazo lililo katika ubeti wa shairi.
- kipande
ni mgao au kisehemu
kimojawapo katika visehemu viwili au vitatu vya mshororo
ambavyo
hutenganishwa kwa kituo au alama ya mkato mwishoni mwa kipande cha kina. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa:
kipande ni kisehemu kimojawapo katika visehemu viwili au zaidi vya kila mstari
kwa tungo zenye kugawanyika katika sehemu mbili au zaidi katika kila mstari.
Mfano:
kila usilolijuwa,
kujifunza ni wajibu,
Ndipo utapo tambuwa,
japokuwa taratibu,
Papara kuiondowa, ili
usije haribu,
Bila shaka utaswibu, ile haja
utakayo.
Katika
ubeti huu kuna vipande viwili ambavyo ni ukwapi na utao.
- ukwapi
ni
kipande cha kwanza cha mshororo.
Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.
Ukwapi umekolezwa vizuri ili uweze kuonekana
vuzuri.
- utao
ni kipande cha pili katika mshororo.
Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu. Utao umekolezwa vizuri.
- mwandamizi
kipande
cha tatu katika mshororo.
Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.
Mwandamizi umokolezwa ili
kuonekana vizuri.
- mizani
ni
silabi zilizomo katika kila mshororo wa shairi huleta urari wa mapigo katika shairi, arudhi huwa na idadi ya mizani
inayolingana. Wamitila (2010:218), anaeleza kuwa mizani ni silabi zinazo tamkika. TUKI (2003:94), mizani
ni jumla ya silabi zilizomo katika kila mstari wa ubeti. Wanafafanua kuwa
katika ushairi hizi ndizo ziletazo urari wa mapigo, kwani kila mstari watakiwa
uwe na mizani sawa na mistari mingine au wakati mwingine ule mstari wa mwisho
uwe na nusu ya mizani ya mstari mmoja. Mashairi yana vipimo vinavyopima urefu
wa kira mstari. Vipimo hivyo huitwa mizani, kila silabi moja Tazama mfano kutoka katika shairi hili; mtunzi
(kapele. H, 2013)
mja deni utalipa,
hata likiwa ni mia,
dawa ya deni kulipa,
wala siko kukimbia,
deni harusi kukopa,
kulipa wafikiria,
ili moyo uwe shwari,
mja kamilisha deni.
Katika
shairi hili mizani iko kumi na sita ambayo inaweza kuonekana hivi na kuhesabika
kwa urahisi.
M ja
de ni u ta li pa,
ha ta
li ki wa
ni mi a,
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16
- urari wa mizani
ni
mpangilio wa idadi ya mizani katika mstari au mshororo mmoja wa shairi. Katika
mashairi ya tarbia (unne), kwa kawaida kuna mizani kumi na sita. Katika tungo
za aina nyingine vipande na mistari huwa na idadi tofauti ya mizani. Mizani
yaweza kuwa irabu moja, konsonanti moja, konsonanti moja na irabu, konsonanti
mbili na irabu, konsonanti tatu na irabu. TUKI (2003:104) wanaeleza kuwa:
urari
ni mpangilio wa mistari ya ubeti. Yaani unaweza kuusoma ubeti halafu ukasema
mstari huu wa pili ungekuwa wa kwanza na huu wa kwanza ungekuwa wa pili.
- kina
ni
sauti ya silabi iliyomwishoni mwa mshororo au kipande cha sauti, kuangalia vina
tunakuta kuna aina mbili ambazo kina cha ndani na kina nje au kina
kati
na kina mwisho. Baadhi ya mashairi yana vina vya kati na vin avya mwisho, yaani
mshororo huwa umegawanyika sehemu mbili, kila sehemu ikiitwa kipande.
Mfano:
hebu tuangalie vina katika shairi lifuatalo, wamitila (2010:218), yeye anaeleza
kuwa vina ni silabi zinazofanana na ambazo hupatikana katika sehemu moja katika
mpangilio wa shairi. TUKI (2003:93), wanaeleza kuwa vina ni zile mizani za kati
na za mwisho au pengine za mwisho tu
zenye kufanana katika kila mstari wa ubeti, na katika tarbia aghalabu
vina hufanana katika ile mistari mitatu ya mwanzo tu, mwanzo, mroto, na mleo. Tazama mfano huu (Kapele. H, 2013)
Tulipofika mpanda, tulizani njia panda,
Tuliendelea panda,
tukaufika uwanda,
Alikozaliwa pinda,
mnyoosha walopinda,
Hongera waziri panda,
sasa twaweza pumua.
TUKI (2003)
Mkono inuka, inuka hima, twaa
kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema,
hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima,
yalipo humu.
Katika
ubeti huu ambao ni mfano mzuri wa shairi la kimapokeo lenye sifa ya tarbia
yaani unne vina vimekolezwa wino na kuonekana wazi. Vina kati ni nda na vina mwisho ni nda. Laini katika mshororo wa mwisho
kina kati ni nda na kina mwisho ni a
- utoshelezi
katika
kujadili utoshelezi waandishi wengi wanaeleza kuwa lazima kila ubeti huitaji
kuwa na maana inayojitosheleza au
kujisimamia bila kutegemea ubeti unaotangulia au unaofuata hapohapo na kuwa na
mtiririko mzuri wa habari inayoelezwa. TUKI (2003:105) wanasema utoshelezo
katika shairi la Kiswahili ni lile ambalo kila ubeti unajitosheleza kamili kwa
habari au ujumbe unaompa msomaji ili afahamu wamweleza nini katika ubeti ule, halafu
uendelee na ubeti mwingine ukiwa katika mtiririko wa habari yako unayoieleza
huku ukiwa mwenye kufuata mpango uleule wa kila ubeti kujitosheleza mpaka
mwisho wa shairi lako.
- muwala
ni
mtiririko wa fani n amawazo ulion amantiki katika shairi, katika taaluma hii ya
ushairi kuna aina mbili za muwala yaani mawazo y aubeti yawe yanafuatana kwa
ufasaha kutoka fatahi, mroto, mleo na kituo ili kuyajenga mawazo kikamilifu.
Aina ya pili au sheria muwala lazima uwe na mtiririko mzuri wa mawazo kutoka
ubeti hadi ubeti katika aina hii mawazo huwa yamefungamana na maudhui ya tungo
huwa yamekamilika. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa muwala ni ile hali ya
utoshelevu katika ubeti hadi ubeti katika utungo mzima, yaani kilaheleza katika
maana lakini wakati huo huo ukawa hausigani na beti nyingine. Mfano ubeti wa
utangulizi wa shairi hauwezi ukawa kati ya utungo. Tazama (Kapele. H, 2013)
hodi hodi naingia, uwanjani
kwa kishindo,
uwanja naufagia, machafu
kuweka kando,
watu wote shangilia, taratibu wangu mwendo,
kinda manua mdomo, chakula
utapikiwe.
Ubeti huu ni mwanzo wa utungo unafaa kuwekwa mwanzo ili
kujua utangulizi wa utungo.